Ukisikia maajabu makubwa ambayo hufikirii kukutana nayo hapa duniani hii ni moja wapo, Kuna mbuga moja ya kufugia nyoka wakubwa inatoa huduma ya “massage” kwa binadamu kwa kutumia nyoka hao “giant pythons” lakini kabla ya kuanza zoezi hilo nyoka hao hulishwa kuku ambao idadi yao hufikia 10 ili wasije kusikia njaa katikati ya shughuli hiyo.